CAAT History

PREAMBLE:

Wazo la kuanzisha chama lilianza mwaka 2009/2010 kwa watanzania wachache waliosomea China kwa kuanza kukutana kwenye vikao vilikuwa vinafanyika New Africa Hotel. Baadaye pia, vikao vilikuwa vikifanyikia Beijing Restaurant, Mikocheni.

MKUTANO MKUU WA KWANZA:

Mkutano mkuu wa kwanza wa chama (General Assembly) ulifanyika Jumapili ya tarehe 14-Nov-2010 katika ukumbi wa Rombo Green View Hotel, Sinza/Ubungo, Dar-es-Salaam (ambao hivi sasa unaitwa Rombo Hotel).

Mkutano huu mkuu ulifanya maazimio kadhaa ikiwemo kutengeneza katiba rasmi ya chama ambayo ingetumika kwenye usajili wa chama. Mkutano huu mkuu uliunda timu ya uongozi ya watu 10 itakayosimamia majukumu hayo.

 

Awamu ya kwanza ya uongozi ya CAAT (2010-2016) iliongozwa na;

 • Eng Fred Maiga (Mwenyekiti)
 • Dr Haji Mwita (Makamu Mwenyekiti)
 • Eng Mosses Swai (Katibu)

na Wajumbe:

 • Dr Paul Peter Mhame
 • Dr George Oreku Ponera
 • Ally Kacheuka
 • Eng Francis Mugisha
 • Eng Gustav Sanga
 • Hawa Ngasongwa
 • Dr Uwesu Mchepange

 

UZINDUZI RASMI:

Sherehe za uzinduzi/ufunguzi rasmi wa chama zilifanyika Alhamis ya tarehe 11-Aug-2011 katika ukumbi wa Karimjee, Dar-es-Salaam. Mgeni rasmi alikuwa balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania H.E. Liu Xinsheng

 

 

 

 

UONGOZI WA MPITO

Jumamosi ya tarehe 20-Feb-2016 ulifanyika mkutano mkuu katika katika eneo la New Msasani Club.

Mkutano huu ulipitisha azimio la kusajili CAAT katika wizara ya Mambo ya Ndani kama chama cha kijamii (society). Mkutano huu ulichagua uongozi/kamati mpya ya kusimamia usajili huo na baadaye kuandaa mkutano mkuu mwingine wa kuchagua viongozi rasmi Viongozi wa mpito waliochaguliwa ni;

 • Dr Paul Peter Mhame (Mwenyekiti)
 • William Kaijage (Makamu Mwenyekiti)
 • Dr George Oreku (Katibu Mkuu)
 • Johnspeter Majura (Naibu Katibu Mkuu)
 • Ponera Ally Kacheuka (Naibu Katibu Mkuu)
 • Shija Boniphace Bundala (Mweka Hazina)

 

SHEREHE ZA MIAKA 6

Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 ilifanyika sherehe/maadhimisho ya kutimiza miaka 6 ya CAAT ilifanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay .

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na jumla ya watu 200.

Mgeni rasmi wa sherehe hiyo alikuwa Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo).

Wageni wengine wa heshima walikuwa Counselor Gao Wei wa ubalozi wa China (ambaye alikuwa anamuwakilisha balozi Dr Lu Youqing) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial Research Developments Organization-TIRDO) Prof Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo.

USAJILI RASMI

Baada ya kutimiza vigezo vyote, China Alumni Association of Tanzania (CAAT) ilipata barua rasmi ya kukubaliwa kusajiliwa tarehe 17-May-2016 kutoka kwa msajili wa vyama wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Chama cha CAAT kilisajiliwa rasmi na wizara ya mambo ya ndani kwa kupata cheti cha usajili namba S.A. 20610 cha tarehe 01-Jun-2016. CAAT imesajiliwa kama chama cha kijamii kwa mujibu wa sheria ya Societies Act [CAP. 337 R.E. 2002]

 

 

 

 

 

ABOUT CAAT

CAAT dedicates to provide a common forum for fostering & promoting friendly fellowship, professional development & socioeconomic endeavors of Tanzanian professionals who graduated in China, as well as acting as a bridge linking the people of the two countries.

Top